Ryakitimbo memorial fund ni taasisi binafsi yenye mipango ya kujenga tabia miongoni mwa watanzania kuchanga kwa ajili ya kuwezesha wake wenye matatizo yasiyozuilika kwa wao pekee yao bila msaada wa wanadamu wenzao.
Neno wafadhili limezoeleka katika jamii zetu za kiafrika, na hii inamaanisha kuwa wazungu au watu kutoka nje ya nchi ndo wanaweza kuchangia misaada ya kuwasaidia ndugu zetu wenye kuishi mazingira hatarishi na magumu. Mfano kuna vijana hawana kazi, kuna yatima hawana msaada wa mahitaji ya msingi, kuna watu wenye ulemavu wa viungo, wajane wasio na mitaji na mbinu za kuzalisha mali, na wengineo wengi wenye kukwama na kukosa uwezeshwaji.
Ryakitimbo memorial fund ina malengo ya kuwashawishi watanzania na waafrika kwa ujumla kuanza tabia ya kuchangia kupitia kununua bidhaa na harambee za aina hiyo, ifike hatua hata sisi tujiite wafadhili wa ndani ya nchi kwa maana tusaidie makundi yenye kuhitaji msaada wetu wa Hali na mali.
20 years death anniversary of the late J.M.M Ryakitimbo( Sept 1994-Sept 2014) is to take off on September 2014 at Ikizu Nyamswa.
ReplyDelete